Africa

Simba vs Al Ahly, Yanga vs Mamelodi Ligi mabingwa Afrika

KLABU ya Simba imepangwa kumenyana na Al Ahly ya Misri katika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika wakati Yanga itakutana na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

Hayo yamefahamika leo Cairo, Misri wakati wa droo ya kupanga michezo ya robo fainali ya Ligi Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Afrika.

Katika robo fainali hiyo TP Mazembe itavaana na Petro Atletico de Luanda ya Angola wakati Esperance de Tunis ya Tunisia itachuana na ASEC Mimosas ya Ivory Coast.

Michezo hiyo itafanyika kati ya tarehe 29 na 30 Aprili, 2024.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button