Ligi Ya Wanawake

Simba Queens Vs JKT Queens Samia Women’s

DAR ES SALAAM: DROO ya mashindano ya Kombe la Samia Women’s imefanyika leo, ikipanga mechi za nusu fainali zitakazochezwa Machi 4 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.

Katika nusu fainali ya kwanza, Simba Queens itavaana na JKT Tanzania, huku nusu fainali ya pili ikihusisha Fountain Gate FC dhidi ya Yanga Princess. Mechi hiyo ya pili imeratibiwa mahsusi kwa ajili ya kuadhimisha Siku ya Wanawake.

Mshindi wa nusu fainali ya kwanza atakutana na mshindi wa nusu fainali ya pili katika fainali, huku timu zitakazopoteza zikicheza mechi ya kutafuta mshindi wa tatu.

Kwa mujibu wa Meneja wa Mashindano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Baraka Kizuguto, mashindano hayo yataanza rasmi Machi 4. Mechi ya kutafuta mshindi wa tatu itachezwa Machi 6, huku fainali ikiandaliwa Machi 8, siku ambayo pia itakuwa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wanawake.

“Fainali na mchezo wa mshindi wa tatu zitafanyika Machi 6 na 8. Tarehe 8 itakuwa maalum kwa ajili ya kutoa zawadi kwa washindi na bingwa wa mashindano haya,” amesema Kizuguto.

Related Articles

Back to top button