FA

Simba na kibonde, Yanga mwendo wa wanajeshi

DAR ES SALAAM : DROO ya hatua ya 32 bora ya Kombe la Shirikisho la CRDB 2025/2026 imetangazwa leo, ambapo Simba, Yanga na Azam FC zimeangukia kwa wapinzani wanaoshiriki ligi ya Championship.

Katika droo hiyo iliyochezeshwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Azam Media, Simba inatarajia kucheza na kibonde kwenye Championship B19 huku Yanga ikikabiliwa na Polisi Tanzania, na Azam FC ikichuana na Mbeya Kwanza.

Timu hizo zikitinga hatua ya 16 bora, Simba itakutana na Dodoma Jiji au African Sports, Yanga itakutana na Tanzania Prisons au TMA Stars na Azam FC Fountain Gate au Gunners FC.

Miongoni mwa mechi nyingine zinazotarajiwa kuchezwa ni Mbeya City dhidi ya Bandari Tanzania, Fountain Gate ikikabiliana na Gunners FC, pamoja na TRA United dhidi ya Kijiwe Nongwa.

Pia, Tanzania Prisons watacheza dhidi ya TMA Stars, na Dodoma Jiji wanakutana na African Sports.

Mechi zingine ni Pamba Jiji FC vs Transit Camp, Mtibwa Sugar vs Mbuni FC, Mashujaa FC vs Kengold, Singida Black Stars vs Songea United, Geita Gold vs Nyika FC, JKT Tanzania vs Hausung FC, Coastal Union vs Stand United, na Namungo vs Kagera Sugar.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button