Africa

Adolf Bitegeko atua Kaizer Chiefs

JOHANNESBURG: Klabu ya Kaizer Chiefs imetangaza kumnasa kiungo wa kati, Adolf Mtasingwa Bitegeko kutoka Azam FC.

Kaizer maarufu Glamour Boys imemtangaza mchezaji huyo leo Jumanne baada ya kufanikiwa kumalizana na Azam huku ada ya usajili ikiwekwa siri.

Kujiunga kwa Adolf, 27 katika timu hiyo inamfanya kuwa mchezaji wa taifa la 20 kuvaa jezi ya kikosi hicho huku akiwa Mtanzania wa kwanza kukipiga Amakhosi.

“Tunamkaribisha kwa mikono miwili Adolf katika familia hii na kumtakia mafanikio katika safari yake na Glamour Boys,” ilieleza sehemu ya taarifa ya Kaizer ya kumkaribisha kiungo huyo.

Adolf anatua Kaizer baada ya kuitumikia Azam kwa misimu miwili na nusu ambapo kabla ya hapo alikipiga ligi za Iceland, Norway na Finland.

Related Articles

Back to top button