Muziki

Baba wa Meja Kunta kuzikwa leo Dar es Salaam

DAR ES SALAAM: Baba mzazi wa msanii wa muziki wa Singeli, Meja Kunta, anatarajiwa kuzikwa leo, Julai 22, 2026, katika Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam kuanzia saa 10 jioni.

Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake kufuatia msiba huo, Meja Kunta alisema baba yake alifariki dunia Julai 21, 2026, baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu (presha).

Msanii huyo alieleza kuwa ugonjwa huo umekuwa ukichangia vifo vya baadhi ya ndugu katika familia yao, jambo lililoongeza majonzi kwa wanafamilia.

Meja Kunta amesema familia imeupokea msiba huo kwa huzuni kubwa na kuwaomba Watanzania kuwaombea marehemu ili Mwenyezi Mungu amsamehe dhambi zake na ampumzishe mahali pema peponi.

Aidha, amewashukuru wote walioendelea kuwapa pole na kuwafariji katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao.

Related Articles

Back to top button