Tetesi

Simba meza moja na Mpanzu

DAR ES SALAAM. KATIKA kuhakikisha wanakiboresha kikosi chao, klabu ya Simba wapo kwenye mazungumzo na mshambuliaji kutoka klabu ya AS Vita Club, Elie Mpanzu, ili kupata huduma yake.

Simba ipo kwenye mchakato wa kuboresha timu kwa kufanya usajili mzuri kwa ajili kukiimarisha kikosi, huku ikitarajia kucheza kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao, baada ya kupoteza nafasi ya kwenda ligi ya Mabingwa Afrika.

Taarifa zilizopatikana kutoka chanzo cha kuaminika, kinadai mazungumzo yalianza kufanyika mapema na mambo yakiwa mazuri utakuwa ni usajili wa kwanza kwa wachezaji wapya ambao wanasajiliwa kwa msimu ujao wa mashindano.

Imeelezwa kuwa viongozi wameanza kusuka kikosi cha timu hiyo kwa msimu ujao kwa kuangalia katika nafasi hasa ushambuliaji ilikuwa tatizo ndani ya Simba baada ya kuondoka kwa Mosse Phiri na Jean Baleke.

“Baada ya kuondoka wachezaji hao, wakaletewa Pa Omar Jobe na Fred Michael lakini hawakuonyesha kile kilichotarajiwa na wanasimba, watu waliopewa jukumu la usajili wameanza kuingia sokoni na Mpanzu ni miongoni mwa nyota ambao wako kwenye mazungumzo,” kilisema chanzo hicho.

Spotileo lilimtafuta Meneja wa Idara ya habari na Mwasiliano ya Simba, Ahmed Ally ambaye amesema mipango yao ni kuboresha kikosi suala la nani anasajiliwa hilo lipo kwa watu maalum wanaohusika na masuala ya usajili.

“Ni kweli maboresha yatafanyika lakini suala la usajili ni siri kwa sasa kwa sababu, tunahitaji kuleta vifaa bora kulingana na mapendekezo ya benchi la ufundi na mahitaji ya timu yetu kwa msimu ujao wa mashindano ikiwemo kombe la Shirikisho la Afrikia,” amesema Meneja huyo.

Related Articles

Back to top button