Ronaldo amaliza safari ya Kombe la Dunia kwa machozi, Hispania yatinga robo fainali

DALLAS: Safari ya nguli wa soka duniani, , katika Kombe la Dunia imefikia tamati kwa huzuni baada ya Ureno kuchapwa bao 1-0 na Hispania katika hatua ya 16 Bora.
Bao la dakika za nyongeza lililofungwa na Mikel Merino liliihakikishia Hispania nafasi ya robo fainali, huku Ronaldo akionekana akitokwa na machozi baada ya filimbi ya mwisho, katika mchezo wa mwisho kwake kwenye Kombe la Dunia.
Ronaldo mwenye umri wa miaka 41, ambaye tayari alitangaza kuwa hili litakuwa Kombe lake la Dunia la mwisho, anaondoka akiwa ameweka rekodi nyingi ikiwemo kufunga mabao katika Kombe la Dunia sita tofauti na kufikisha mabao 976 akiwa na klabu pamoja na timu ya taifa.
Hata hivyo, ndoto yake ya kutwaa taji hilo kubwa zaidi duniani haijawahi kutimia.
Baada ya mchezo, Ronaldo hakutangaza rasmi kustaafu timu ya taifa, akisema atakaa na familia yake na kufanya uamuzi kwa utulivu kuhusu hatua inayofuata.
Kocha wa Ureno Roberto Martinez, , naye ametangaza kuondoka mara baada ya timu hiyo kutolewa, akisema alifika nchini humo akiwa na lengo la kushinda Kombe la Dunia na kwa kuwa hakufanikiwa, hana sababu ya kuendelea.
“Mkataba wangu umefikia mwisho. Tulijitahidi kutimiza ndoto ya Ronaldo na taifa la Ureno, lakini haikuwezekana,” alisema Martínez.
Licha ya Ronaldo kufunga mabao matatu katika mashindano haya, kiwango chake kilizua mjadala mkubwa, huku wachambuzi wengi wakihoji uamuzi wa kocha kuendelea kumtumia kama mchezaji wa kikosi cha kwanza.




