La Liga
Rais Barcelona ‘presha’ juu kisa Mbappe
BARCELONA: RAIS wa ya Barcelona Joan Laporta amekiri kwamba kuhamia kwa Kylian Mbappe kwa wapinzani wao Real Madrid si habari njema kwao.
Mbappe amejiunga na Real Madrid kama mchezaji huru akitokea Paris Saint German (PSG) ya Ufaransa.
Akizungumza na Mundo Deportivo Laporta amesema: “Kama shabiki wa Barca, sio habari njema kumuona Mbappé anakwenda Real Madrid.
“Lakini kusema ukweli, ninapendelea mkakati wetu wa kuamini mradi na wachezaji waliozalishwa na kufanywa La Masia.
“Nawaheshimu wapinzani wetu lakini ninahifadhi Falsafa yetu.” Alisema Laporta akipongeza mpango wao wa kuzalisha wachezaji amkinda.
Mbappe atavaa jezi namba 9 Bernabeu baada ya kujifunga jela ya Bernabeu kwa miaka mitano ambapo pia atavuna mamilioni ya pesa.