Kwingineko

PSG Yamnasa Willian Pacho

PARIS: Klabu ya Paris Saint- Germain imetangaza kukamilisha usajili wa mchezaji Willian Pacho (22) kutoka klabu ya Eintracht Frankfurt kwa dau linalokadiriwa kuwa Euro milioni 45.
Pacho anawasili klabuni hapo kuitumikia kwa mkataba wa miaka mitano ikiwa ni mpango wa klabu hiyo kujenga kikosi imara kwa miaka ijayo.
Pacho ni beki ambaye anatajwa kuja kuwa mmoja kati ya mabeki bora siku za usoni, na hiki ndio kitu kilichowafanya PSG kumwaga pesa nyingi kwake na ilielezwa kwamba klabu kadhaa zilikuwa zikimuwinda ikiwemo Liverpool.

Related Articles

Back to top button