Tetesi

Pauni milioni 81 kumng’oa Alvarez City

KLABU ya Atletico Madrid imekubali dau la £81.5m kuinasa saini ya mshambuliaji Julian Alvarez kutoka Manchester City.

Dau la Alvarez imeripotiwa kuwa £64.4m (75m euros) na nyongeza ya £17.1m (20m euros) ‘add-ons’.

It would be a record sale for City, surpassing the £50m Chelsea paid for Raheem Sterling in 2022.

Hii itakuwa rekodi ya mauzo kwa City, ikiipita ile ya Raheem Sterling ya £50m kwenda Chelsea msimu wa 2022.Kwa mujibu wa BBC, Alvarez alitakiwa kutoa maamuzi yake bada ya Argentina kuondolewa kwenye michuano ya Olympics.

Kocha wa City, Pep Guardiola amesema amekuwa akitamani Alverez ,24, abaki na kuongeza kuwa mwanzoni mwa mwezi huu alimuhesabu nyota huyo kwenye orodha ya wachezaji watakaounda kikosi chake msimu huu wa EPL.

“Namjumuisha, ila amesema maamuzi yote yatatoka tukiwa pamoja. Lakini, kama ilivyokuwa siku za nyuma kwa Ilkay Gundogan, Riyad Mahrez na Aymeric Laporte, City haitamzuia mchezaji anayetaka kuondoka,” alisesema Guardiola.

Muargentina huyo, ambaye alijiunga na City mwaka 2022 kwa mkataba wa pauni milioni 14.1 kutoka River Plate, amefunga mabao 36 katika mechi 106 akiwa City.

Alvarez alishinda ‘treble’ katika msimu wake wa kwanza Etihad na mshambuliaji huyo alishiriki katika ushindi wa Argentina Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar na Copa America 2024 nchini Marekani.

Related Articles

Back to top button