Mahusiano

Paula: Marioo amenipenda jinsi nilivyo

DAR ES SALAAM: PAULA Paul ‘Paula Kajala’ amesema hapendi kutegemea make up katika maisha yake ya kila siku, akieleza kuwa anajiamini katika mwonekano wake wa asili na hana tabia ya kushindwa kutoka nyumbani kwa sababu hajajipamba.

Paula ameyasema hayo alipokuwa akizungumza kuhusu mtazamo wake juu ya matumizi ya make up, ambapo amesisitiza kuwa kwake si jambo la msingi au kipaumbele katika maisha ya kila siku.

“Kwa sababu mimi ni mzuri,” amesema Paula kwa kujiamini alipoulizwa kwa nini hapendi kupaka make up mara kwa mara.

Amesema kuwa wapo baadhi ya watu hutumia make up kuficha vitu wasivyovipenda kwenye muonekano wao, Paula amesema baadhi yao hukosa kujiamini.

“Ndiyo, wengi wao hawajiamini. Mimi siyo kwamba sipaki make up kabisa, napaka mara moja moja, lakini kwangu make up siyo kipaumbele,” amesema.

Ameongeza kuwa hawezi kushindwa kutoka nyumbani kwa sababu tu hajapaka make up.

“Yaani mfano ukute siwezi kutoka nyumbani kwa sababu sijapaka make up? Hapana, hilo haliwezekani. Naweza nisivae make up lakini nikatoka vizuri tu,” amesema.

Paula pia alifichua kuwa wakati mwingine anapopaka make up, mpenzi wake na msanii wa Bongo Fleva, Marioo, hupenda kumtania kutokana na jinsi anavyoupenda mwonekano wake wa asili.

Paula amesema kwa upande wake, Marioo hampendi Paula apake make up mara kwa mara, amesema anaona mrembo huyo anavutia zaidi akiwa katika muonekano wake wa kawaida.

“Mimi naona Paula anakuwa mzuri zaidi akiwa hajapaka make up,” amesema Marioo.

Kauli za wawili hao zimmevutia mashabiki wao, huku wengi wakisifu kujiamini kwa Paula na namna ambavyo Marioo anavyounga mkono mwonekano wake wa asili.

Related Articles

Back to top button