Mahusiano

Tom Cruise, Maha Dakhil, yamewakuta!

LONDON: Tom Cruise alikuwa amezua tetesi za uhusiano na wakala wake wa muda mrefu, Maha Dakhil, baada ya wawili hao kuonekana kwenye chakula cha jioni huko London hivi karibuni.

Tom na Maha walionekana kwenye chakula cha jioni na ripoti zilidai kuwa walionekana wakigusana mno jambo ambalo lilizua uvumi huo huku wengi wakidhani kwamba wangechumbiana, lakini taarifa kutoka vyanzo vya taarifa hizo zinadai kwamba wawili hao hawawezi kuwa katika uhusiano wa kimapenzi kwa sababu wote wanawapenzi wanaowapenda mno.

“Maha Dakhil ameolewa ana mume anayempenda na wanafuraha katika mapenzi yao hivyo hivyo kwa Cruise hawezi kuvuka mipaka ya kutoka na Maha kwa sababu wote wanamahusiano yao na yapo vizuri,” Chanzo hicho kilieleza kwamba, “Tom na Maha wanapendana sana lakini ni marafiki tu.”

Taarifa za awali za wawili hao zilitokana na picha zilizopigwa Desemba 18 zikiwaonesha wawili hao wakiwa katika chakula cha jioni katika mgahawa wa Mayfair mjini London. Minong’ono ilianza huku wengi wakidai wawili hao walijiachia mno kwa starehe.

“Ile ni picha tu lakini wawili hawa hawawezi kuchumbiana kwa sababu hizo chakula hicho kilikuwa kwa marafiki wawili wanaofanyakazi pamoja na waliamua kutoka kwa ajili ya kupongezana kwa kazi zao zilizotukuka,” Chanzo hicho kiliendelea kueleza.

Related Articles

Back to top button