Madereva Formula One waogopeshwa na dola milioni 96

MADRID, Hispania: MADEREVA wa Formula One wanatarajia wikendi yenye presha, ajali na ushindani mkali katika mashindano ya ‘Circuito de Madring’ utakaofanyika kama Spanish Grand Prix kwa mara ya kwanza.
Licha ya kuwa ni mzunguko mpya kwenye kalenda ya mashindano hayo, tayari umeibua hofu miongoni mwa madereva kutokana na muundo wake wenye changamoto na kasi kubwa.
Dereva wa Alpine, Pierre Gasly, ambaye alishinda nafasi ya kwanza mashindano ya Italian Grand Prix ya Monza. “Nitaweka dau langu kwenye red flag,” alisema Gasly, akimaanisha kusimamishwa kwa mbio kutokana na ajali au tukio kubwa. Kauli hiyo inaonesha kiwango cha tahadhari kilichopo kabla ya magari kuanza kuingia rasmi kwenye ushindani.
Mzunguko huo wenye urefu wa kilomita 5.416 umejengwa kwa gharama ya zaidi ya euro milioni 83, sawa na takribani dola milioni 96. Siku ya Alhamisi, madereva walitembea kuuzunguka mzunguko huo kwa umakini, wakichunguza kona, sehemu za kasi na maeneo ambayo yanaweza kuwa hatari. Kwa wengi wao, huu si mzunguko wa kawaida, bali ni mtihani mpya unaohitaji umakini wa hali ya juu.
Colapinto anaamini Madring imekusanya karibu kila aina ya changamoto ambazo dereva anaweza kukutana nazo katika mbio za Formula One.
Kwa upande mwingine, dereva mkongwe wa Cadillac, Sergio Perez, mwenye uzoefu wa mbio 294 za Grand Prix, alielezea mzunguko huo kwa neno moja: “Unatisha!” Perez alilinganisha mazingira yake na mzunguko wa Jeddah, akisema ni wa kasi, mzuri na wa kiwango cha juu. Pamoja na hofu hiyo, Mmexico huyo amesema anafurahishwa kuwa sehemu ya tukio hilo na anaamini mashabiki watafurahia mashindano hayo.




