Mastaa

Otile: Jovial asije kwenye msiba wangu

NAIROBI: UGOMVI baina ya wasanii Otile Brown na Jovial umefikia pakubwa baada ya Otile kutotaka Jovial ahudhurie kwenye msiba wake.

Otile ametoa kauli hiyo baada ya majibizano yanayoendelea mitandaoni baina yao kila mmoja akimshutumu mwenzake kuwa chanzo cha tatizo.

Akizungumza na Tony Mwirigi ambaye ni mtangazaji wa Kenya, Otile amesema ameumizwa na kauli alizozitoa Jovial katika mgogoro wao baada ya kufanya kazi pamoja kwa muda mrefu, ndio maana amefikia uamuzi huo.

“Kuhusu Jovial nasema leo hii kwamba hata ikitokea nimefariki, Jovial hapaswi kuruhusiwa kuingia kwenye msiba wangu, yaani hapaswi kuruhusiwa kuhudhuria mazishi yangu. Yaani ndio mambo yamefika mbali kiasi hicho,” alisema Otile.

Otile alimtambulisha Jovial katika muziki baada ya kumsaini kwenye lebo yake ya Just In Love Music mwaka 2019.

Wawili hao walitengeneza ngoma kali kadhaa za kushirikiana pamoja zikiwemo Jeraha, Ulinihukumu, Zichune, Such Kinda Love na nyingine kabla ya kuhitirafiana na Jovial kuondoka katika lebo hiyo.

Hata hivyo, vita ya maneno iliendelea kurindima baina yao mitandaoni kila mmoja akimshutumu mwenzake kutomtendea haki wakati wakishirikiana kimuziki kabla ya Otile kuibuka na kauli hiyo mpya.

 

Related Articles

Back to top button