Nyumbani

BASATA na China kuimarisha kushirikiano wa kisanii fursa za kimataifa 

DAR ES SALAAM:BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) na Ubalozi wa China nchini Tanzania zimejadili namna ya kuimarisha ushirikiano katika sekta ya sanaa, hatua inayolenga kufungua fursa zaidi kwa wasanii wa Tanzania kupata majukwaa ya kimataifa, kubadilishana uzoefu na kukuza ubunifu.

Hatua hiyo imekuja kufuatia mazungumzo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam kati ya Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA, Edward Buganga, na Counselor Qiangqing Li wa Ubalozi wa China nchini Tanzania.

Mazungumzo hayo yamefanyika katika ofisi za Ubalozi wa China jijini Dar es Salaam, ambapo Buganga aliambatana na maafisa mbalimbali kutoka BASATA.

Katika mazungumzo hayo, pande hizo zimejadili fursa za kuimarisha ushirikiano wa kisanaa kati ya Tanzania na China, hususan katika kukuza na kuendeleza sekta ya sanaa kupitia kubadilishana uzoefu, utaalamu na maarifa.

Aidha, ushirikiano huo unalenga kufungua milango zaidi kwa wasanii wa Tanzania kushiriki katika majukwaa ya kimataifa, kupata fursa mpya za kujitangaza na kuendeleza vipaji vyao katika soko la sanaa la kimataifa.

Ushirikiano kati ya Tanzania na China katika eneo la sanaa pia unaweza kuwa chachu ya kukuza mwingiliano wa tamaduni, ubunifu na fursa za kiuchumi zinazotokana na sekta ya sanaa na ubunifu.

Kupitia mazungumzo hayo, BASATA na Ubalozi wa China wameendelea kuweka msingi wa ushirikiano utakaosaidia kuimarisha mahusiano ya kisanaa na kufungua fursa mpya kwa wadau wa sanaa kutoka mataifa hayo mawili.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button