AfricaAfrika Mashariki

Ni Tanzania vs Zanzibar CECAFA U15

TIMU ya taifa ya viijana wenye umri chini ya miaka 15 leo itaikabili Zanzibar katika mchezo wa mwisho wa kundi B michuano ya Shirikisho la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati inayoendelea Uganda.

Mchezo huo utafanyika uwanja wa FTC Njeru uliopo Jinja. Tayari Tanzania na Zanzibar zimetinga nusu fainali.

Katika michezo iliyotangulia Tanzania imezifunga Rwanda mabao 2-1 na Somalia bao 1-0 wakati Zanzibar amezifunga Somalia mabao 4-0 na Rwanda 3-0.

Related Articles

Back to top button