Muziki

Ndugu wa Michael Jackson kafa Sept15 kazikwa Nov 4

CALFONIA: WATOTO wa Michael Jackson Paris na Bigi Jackson wametoa heshima zao za mwisho wakati mjomba wao Tito Jackson alipozikwa jana Novemba 04, 2024 tangu alipofariki September 15, 2024 akiwa na miaka 70.

Mazishi ya Tito yamefanyika katika makaburi ya Forest Lawn huko Glendale, California nchini Marekani.

Shangazi wa Paris na Bigi La Toya Jackson mwenye miaka 68, mjomba Marlon Jackson mwenye miaka 67 na binamu yake Jaafar mwenye miaka 28 pamoja na Jermajesty mwenye miaka 24 pia walitoa heshima zao kwa Tito kabla ya kuzikwa kwake.

Nyota huyo wa Jacksons, Tito kaka mkubwa wa aliyekuwa Mfalme wa Pop Michael Jackson, ambaye alifariki mwaka 2009 akiwa na umri wa miaka 50 alipatwa na mshtuko wa moyo wakati akiendesha gari kutoka New Mexico hadi Oklahoma mwezi Septemba.

Baada ya kifo cha Tito, Paris aliweka picha yake na baba yake marehemu Michael kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Aliandika: “Rest katika mpito Uncle Tito.”

Tito, ambaye alikuwa kaka wa marehemu Mfalme wa Pop Michael na dada yake Janet mwenye miaka 58, alijipatia umaarufu pamoja na kaka zake kwenye Jackson 5 ambao baadaye walikuja kuwa Jacksons mwishoni mwa miaka ya 1960 na 1970 chini ya lebo ya Motown.

Kundi la The Jacksons pia linaundwa na ndugu wa Tito Marlon mwenye miaka 67 na Jackie mwenye miaka 73,

Nyimbo zao maarufu zaidi ni pamoja na ‘ABC’, ‘The Love You Save’, na ‘I’ll Be There’.

Tito aliingizwa kwenye Rock and Roll Hall of Fame kama mshiriki wa Jackson 5, na akina Jackson walipokea nyota kwenye ‘The Hollywood Walk of Fame’ mwaka wa 1980.

Akiwa mwimbaji na mpiga gitaa alianza kazi ya peke yake mnamo 2003 kama mwanamuziki wa blues.

Related Articles

Back to top button