Mastaa

Mwanamke anaswa kwa kufyatua risasi karibu na nyumba ya Rihanna

LOS ANGELES: Polisi wa Los Angeles wamemkamata mwanamke mwenye umri wa miaka 35 baada ya kufyatua risasi karibu na nyumba ya mwanamuziki maarufu Rihanna katika eneo la Beverly Hills huko Marekani.

Kwa mujibu wa polisi, tukio hilo lilitokea majira ya saa saba mchana, baada ya kupokea taarifa kuhusu milio ya risasi katika eneo hilo. Mwanamke huyo alikamatwa bila tukio lolote la ziada huku silaha iliyofyatuliwa ikipatikana.

Hakuna mtu aliyejeruhiwa katika tukio hilo, na haijafahamika mara moja iwapo Rihanna alikuwa nyumbani wakati wa tukio hilo.

Mshukiwa huyo anashikiliwa gerezani kwa tuhuma za jaribio la mauaji huku akitakiwa kuweka dhamana ya dola milioni 10 wakati uchunguzi ukiendelea.

Related Articles

Back to top button