Filamu

Muongoza filamu wa Marekani adai viumbe wa angani wameshafika duniani

LOS ANGELES: MTAYARISHAJI na mwongozaji maarufu wa filamu aliyeshinda tuzo za Oscar, Steven Spielberg, amesema anaamini viumbe kutoka sayari nyingine wamewahi kufika katika sayari ya dunia na huenda baadhi yao wapo hadi sasa.

Spielberg alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza katika kipindi cha CBS Sunday Morning wakati akitangaza filamu yake mpya ya kisayansi inayojulikana kama ‘Disclosure Day’.

Akizungumzia suala la viumbe wa angani, Spielberg alisema ushahidi mbalimbali aliokusanya kwa miaka mingi pamoja na ushuhuda uliowahi kutolewa mbele ya Bunge la Marekani umemfanya kuamini kuwa viumbe hao wapo.

“Ninaamini kabisa wamewahi kufika hapa duniani na huenda bado wapo,” alisema Spielberg.
Licha ya kuongoza filamu nyingi zinazohusu viumbe wa angani, Spielberg amesema hajawahi kushuhudia tukio lolote la ajabu linalohusishwa na viumbe hao.

Filamu yake mpya ‘Disclosure Day’ inatarajiwa kuonyeshwa rasmi kimataifa Juni 12 na inahusu njama zinazohusisha UFO pamoja na siri za uwepo wa viumbe kutoka sayari nyingine.

Related Articles

Back to top button