Filamu

Filamu ya ‘The Battle for Laikipia’ kufungua Tamasha la Filamu la NBO

NAIROBI: TAMASHA la Filamu la NBO toleo la 5 linatarajiwa kufanyika kuanzia Oktoba 17 hadi 27 mwaka huu wa 2024.
Tamasha hilo litafanyika katika eneo la Prestige Cinema kwenye Barabara ya Ngong, huku likipanua mkondo wake kwa maonyesho ya ziada katika kumbi maarufu kote Nairobi.

Sehemu zitakapoonyeshwa baadhi ya filamu wakati wa tamasha hilo ni Jumba la kihistoria la Kaloleni Social Hall huko Eastlands hadi Docubox katika Shalom House, na nyumba ya maonyesho ya sinema huru, Sinema na katikati ya Jiji.

Tamasha la Filamu la NBO linaonyesha filamu za Kenya na Afrika Mashariki ambapo ndani ya siku 10 zitaonyesha filamu 17 mpya ndefu, filamu fupi mpya 22 na maonyesho mawili ya kwanza ya Kenya ya filamu zilizoshinda Tuzo zinazowasilishwa kwa watazamaji kwa mara ya kwanza.

Filamu mbili za Kenya zinazoshughulikia suala muhimu la mzozo wa ardhi ndizo zitazofungua na kufunga tamasha hilo ambapo filamu ya ‘The Battle for Laikipia’ ambayo ni filamu ya uchunguzi wa migogoro ya ardhi inayoendelea nchini Kenya na filamu itakayofunga tamasha hilo ni filamu ya ‘Nchi Yetu, Uhuru Wetu’, ikielezea mapambano ya taifa ya kupigania haki za ardhi, kuchunguza changamano za ardhi, utambulisho na haki.

Mwanzilishi wa tamasha hilo, Sheba Hirst, amesema, “Baada ya kusimama kwa muda mrefu, tunafurahi kurudisha Tamasha la Filamu la NBO katika jiji na eneo la awali. Tutaonyesha filamu zinazozungumzia hisia zetu, kulinda sanaa, ubunifu na uchunguzi wa kina unaweza kustawi.

Sheba amesema filamu nyingine zitakazoonyeshwa ni kutoka Afrika na Diaspora ya Afrika, zikiwemo kazi mashuhuri za watengenezaji filamu wa Afro-European na Afro-Caribbean.

“Kila onyesho litafuatwa kwa kushirikisha vipindi vya maswali na majibu na watengenezaji filamu au mijadala inayowezeshwa ya ‘FilmTalk’, ikitoa maarifa ya kina kuhusu mada za filamu na umuhimu wake kwa hadhira ya sasa.

Related Articles

Back to top button