Nyumbani

Manara: Nimemuachia Mungu

DAR ES SALAAM: Msemaji wa Zamani wa Yanga na Simba Haji Manara amesema anaamini kwamba kila jambo lina wakati wake hivyo hana shaka na uamuzi wa uongozi wa Klabu ya Yanga juu ya nafasi yake klabuni hapo.

Akizungumza na kituo cha Wasafi, Manara amesema amepokea kwa mikono miwili maamuzi ya viongozi wake na yupo tayari kwa majukumu yoyote atakayopangiwa.

Ameongeza kuwa Mungu ndiye anaejua kuhusu hatima yake hivyo kwasasa ameupa muda nafasi wakati ukifika mambo yote yatakuwa hadharani.

Ikumbukwe ni siku mbili tu zimepita tangu Rais wa Yanga Hersi Said atangaze kuwa Haji Manara sio msemaji wa Yanga na atapangiwa majukumu mengine, kauli iliyokuwa gumzo mitandaoni.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button