Kwingineko

Mshahara wamkwamisha De Gea kusajiliwa Genoa

GENOA: KIPA wa zamani wa Manchester United David de Gea hatojiunga na klabu ya Serie A ya Italia Genoa kama ilivyopangwa awali kwa sababu ya kutofikia makubaliano ya mshahara anaotaka.

Mtandao wa talkSPORT umeeleza kwamba mshambuliaji huyo wa Uhispania alipata fursa ya kurejea kwenye soka akiwa na Genoa, baada ya kuwa mchezaji huru kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 alijiunga na Manchester United kwa miaka 12 kabla ya kuondoka Old Trafford mwishoni mwa msimu wa 2022-23.

Mkataba wake na Mashetani Wekundu ulimalizika na alishindwa kuafikiana kuhusu kuongezwa kwa klabu hiyo ya Ligi Kuu ya Uingereza.
De Gea alitumia muda wake mwingi kufanyamazoezi peke yake bila kujiunga na klabu yoyote, licha ya kuwa na nia ya kutaka Kwenda kucheza soka Saudi Arabia na Marekani.

Alikuwa kwenye mazungumzo na Genoa ili kuhamia klabu hiyo lakini kulingana na ripoti ya hivi punde, hatojiunga nao katika dirisha hili la usajili la majira ya kiangazi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button