Elanga atua Forest

TIMU ya Nottingham Forest imemsajili fowadi wa Sweden Anthony Elanga kutoka klabu ya Manchester United kwa mkataba wa miaka mitano.
Inaaminika uhamisho wa Elanga mwenye umri wa miaka 21 kutoka Old Trafford umeigharimu Forest ada ya pauni milioni 15 sawa na shilingi bilioni 45.64.
Elanga amekuwa akicheza United tangu akiwa na umri wa miaka 12 na aliitwa timu ya wakubwa mwaka 2021. Amecheza mechi 55 katika mashindano yote.
“Ni furaha kuwa hapa. Ni wakati wa kujivunia, sio kwangu tu, hata kwa familia yangu pia. Kulikuwa na timu zinanihitaji, lakini kwangu, nahisi Nottingham Forest ni mahali pazuri. Niko tayari kwa changamoto,” amesema Elanga.
Elanga alifunga magoli manne akiwa United na ingawa alishindwa kufunga katika michezo 26 msimu uliopita, alianza katika michezo saba tu.