Mitindo

Mtanzania Anjali Borkhataria aweka rekodi Ufaransa

PARIS, Ufaransa: MWANAMITINDO Mtanzania, Anjali Borkhataria ameendelea kuiheshimisha nchi baada ya kuwa mwanamitindo wa kwanza kutumbuiza kwenye onesho la ‘pop-up’ lililoandaliwa na Galeries Lafayette nchini Ufaransa.

Onesho hilo lililofanyika kuanzia Juni 25 mpaka Julai ni tukio kubwa la lililokutanisha baadhi ya wanamitindo wa Wakiafrika na kushirikisha wabunifu sita wenye vipaji kutoka nchi mbalimbali za Nigeria, Ghana, Ivory Coast, Togo, Morocco, na Tanzania.

Akizungumza na SpotiLEO mapema leo, Anjali Borkhataria amesema wabunifu waliochaguliwa katika hafla hiyo hawakuchaguliwa kwa sababu ni wabunifu wa Kiafrika, ila walizingatia ladha ya kipekee ambayo ingeendana na ukubwa onesho.

‘The pop-up’ ni zaidi ya tukio la mauzo, ni jukwaa la kusherehekea nchi yetu mama, Afrika, na kutambulisha ulimwengu wa vipaji na ubunifu uliopo ndani ya mipaka yetu. Inatoa fursa ya kipekee kwa wateja kununua miundo halisi ya ubora Kiafrika ambayo si maridadi tu bali pia hadithi ya urithi na ufundi wetu,” amesema Anjali Borkhataria.

Anjali amesema tukio hilo linasisitiza umuhimu wa kusaidia mafundi na wabunifu wa ndani na kuangazia ushawishi unaokua wa mitindo ya Kiafrika katika soko la kimataifa lakini ilikuwa sehemeu ya mabadilishano ya kitamaduni yaliyoleta uchangamfu wa wanamitindo na kupamba tukio hilo.

Mbunifu huyo amesema kuwa fursa hiyo inayoheshimika ni ushahidi wa bidii ya wabunifu wa Kitanzania,   na kuthaminiwa kwa wanamitindo wa Kiafrika kwenye maonesho makubwa ya kimataifa.

“Kupata nafasi hapa ni hatua muhimu kwani inaonesha ongezeko la kutambuliwa kwa wabunifu wa Kiafrika kwenye jukwaa la kimataifa la mitindo,” amesema Anjali.

Anjali Borkhataria aliwahi kutajwa kwenye jarida la Forbes Afrika, pia aliwahi kualikwa kwenye mahojiano BBC  London, mwezi Machi aliingia kwenye ushirikiano na Kampuni ya Reebok Afrika Kusini.

Pia amewahi kuwavalisha wasanii Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’  Mbwana Kilungi ‘Mbosso’ Tanasha Dona na Kofi Olomide.

Pia ni Mkurugenzi Mbunifu wa Taasisi ya EKANTIK iliyoanzishwa mwaka 2018 kwa lengo la kutengeneza mavazi sanaa na muundo mzuri.

Related Articles

Back to top button