Guardiola: kufuzu UEFA CL ni muhimu sana

MANCHESTER: Kocha mkuu wa Manchester City Pep Guardiola sasa anasema kufuzu kwa kikosi chake kwenye Ligi yaMabingwa barani Ulaya msimu ujao ni Muhimu sana na watafanya kila kitu kuhakikisha hilo linatokea licha ya mwenendo mbovu wa kikosi chake msimu huu.
Ushindi wa 1-0 wa Man City mbele ya Spurs Jumatano uliwaweka katika nafasi ya 4 na pointi 47 pointi 7 nyuma ya washindi wa pili msimu uliopita Arsenal walio nafasi ya pili na 54, na pointi moja Nyuma ya Nottingham Forest walio katika nafasi ya tatu na Guardiola anaamini wanaweza kumaliza katika nafasi hizo za juu na kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa msimu ujao.
“Kufuzu kwenye Ligi ya Mabingwa ni jambo zuri sana kwa klabu ni muhimu kwa klabu yenyewe, wachezaji wapya na wa zamani huenda isiwe kitu muhimu sana kwenye vitabu vya Historia lakini kwetu ni muhimu, ni fursa ya kutwaa mataji ambayo hatutaki kikosa”
“Ukilizungumzia hilo ni lazima uwafikirie washindani wetu pia ambao na wao pia wanaitamani nafasi kama hii. Lazima ufikirie klabu kama Forest, Newcastle, Aston Villa, Bournemouth na Brighton ambao kwakweli tumepishana pointi chache sana” amesema.
Manchester City wanatafuta nafasi ya kuwa kwenye michuano hiyo mikubwa barani Ulaya kwa mara ya 15 mfululizo na kufanya hivyo ni lazima watoke jasho.