Nyumbani

Mligo ataja changamoto ya kukosa mashabiki

DAR ES SALAAM: MCHEZAJI wa Simba, Anton Mligo, amesema kikosi hicho kimejipanga kuongeza juhudi katika mchezo wake ujao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya FC 15 de Agosto, licha ya kukosa sapoti ya mashabiki uwanjani.

Mligo amesema benchi la ufundi limefanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza katika mchezo uliopita, huku wachezaji wakiongeza bidii mazoezini kwa lengo la kupata matokeo yatakayoiwezesha Simba kufuzu hatua ya makundi.

Amesema kucheza nyumbani ni faida kwa timu hiyo, lakini kutokuwa na mashabiki uwanjani ni changamoto kwa kuwa uwepo wao huongeza morali na nguvu kwa wachezaji.

“Hata hivyo, tumepokea hali hiyo kama wachezaji na tunatambua kwamba tunahitaji kupambana zaidi kwa sababu hatutakuwa na mashabiki uwanjani,” amesema Mligo.

Ameongeza kuwa kikosi kinaendelea kujiandaa vizuri kwa mchezo huo, huku akiahidi kuongeza juhudi ili kuonesha imani ambayo kocha ameweka kwake na kuisaidia timu kufikia malengo yake.

 

Related Articles

Back to top button