Kwingineko

Mbappé kukosa ufunguzi Ligue 1

FOWADI Kylian Mbappé hatakuwemo kwenye kikosi cha Paris Saint-Germain katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Ufaransa, Ligue 1 dhidi ya Lorient Agosti 12 kwenye uwanja wa nyumbani wa Princes, mtandao wa michezo na burudani, ESPN umesema.

Mbappé hajafanya mazoezi na kikosi cha kwanza chini ya kocha mpya Luis Enrique huku akiwa na mgogoro wa kimkataba na klabu hiyo.

Kwa mujibu wa ESPN, Mbappé anaweza kukosa michezo yote ya PSG mwezi huu dhidi ya Lorient, Toulouse na Lens kama adhabu.

Hivi karibuni Mbappé ameiambia PSG kwamba hataongeza mkataba wake na anapanga kuondoka klabu hiyo Juni 2024 kwa uhamisho huru.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa aliachwa na PSG katika ziara ya Japan ya maandalizi ya msimu mpya huku Rais wa timu hiyo Nasser Al-Khelaifi akitaka ama akubali dili la mkataba mpya utakaomweka zaidi ya Juni 2024 au aondoke majira haya ya joto.

Al Hilal ya Saudi Arabia ni klabu pekee iliyokwisha tuma ombi rasmi kumsajili Mbappé lakini katika hatua ya uhamisho, ana nia tu kujiunga na Real Madrid.

Madrid imekuwa kimfuatilia Mbappé kwa zaidi ya miaka kumi na ilijaribu kumsajili katika kila madirisha mawili ya uhamisho yaliyopita.

Vyanzo vya habari vya ESPN vimesema kwamba PSG inakusudia kumfungia Mbappé katika kikosi cha kwanza kwa msimu mzima asipoongeza mkataba wake lakini mchezaji huyo haonekani kubadili nia yake.

Related Articles

Back to top button