Kwingineko
Kipute Ligi ya Mabingwa Ulaya
MICHEZO miwili ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya(UCL) inapigwa leo Hispania na England.
BARCELONA itakuwa mwenyeji wa Napoli kwenye uwanja wa Olimpico Lluis Companys uliopo Manispaa ya Barcelona.
Katika mchezo wa kwanza timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1 mjini Naples, Italia.
Jiji London, FC Porto itakuwa mgeni wa Arsenal kwenye uwanja wa Emirates.
FC Porto ilishinda bao 1-0 dhidi ya Arsenal katika mchezo wa kwanza uliopigwa Porto, Ureno.