EPL

Marmoush, Ederson wanukia Man City

MANCHESTER:KATIKA hatua za kujiimarisha, mabingwa watetezi wa EPL Manchester City wanawania saini ya Mshambuliaji wa Eintracht Frankfurt Omar Marmoush na mido wa Atalanta Mbrazil Ederson Jose dos Santos da Silva maarufu Ederson.
Gazeti la the Sun la nchini England linaripoti kuwa meneja wa Manchester city Pep Guardiola amewasilisha majina ya wachezaji hao ili wasajiliwe dirisha hili la Januari kuimarisha kikosi chake ambacho kipo kimedhoofika kwa sasa.
Inaelezwa kuwa Matajiri wa Etihad wako tayari kuvunja benki ili kupata saini ya Marmoush kuimarisha eneo la ushambuliaji huku Ederson akitazamiwa kuja kupoza machungu ya kumkosa Rodri.
Marmoush mwenye magoli 18 na pasi 11 za mabao katika mchezo 24 aliyocheza anahusishwa pia na Washika mitutu wa jiji la London Arsenal na vinara wa ligi Liverpool.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button