Man United wakataa ofa ya Fulham kwa McTominay
MANCHESTER, Uingereza: KLABU ya Manchester United ya Uingereza imekataa ombi la kumnunua Scott McTominay kutoka Fulham.
Ofa ya Fulham kwa McTominay inafahamika kuwa ni chini ya pauni milioni 30 ambazo United wamekataa kwa kiungo huyo wa Scotland aliyefunga mabao 10 msimu uliopita.
McTominay, ambaye amevutiwa na Galatasaray, amebakiza mwaka mmoja tu katika mkataba wake lakini United wana chaguo la kuongeza mkataba kwa miezi 12 zaidi.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alikuwa wa kwanza kwa wachezaji waliotoka kwenye Euro 2024 kurejea kwa mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya na anaweza kushiriki katika mchezo wa pili wa Jumamosi dhidi ya Rangers huko Murrayfield.
Wakati huohuo, klabu ya West Ham imeweka dau la kumnunua Wan-Bissaka kwa pauni milioni 15.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 aliigharimu United paundi milioni 50 aliposajiliwa kutoka Crystal Palace mwaka 2019, lakini sasa yuko katika mwaka wa mwisho wa kandarasi yake baada ya na klabu hiyo na anaweza kuondoka bure msimu ujao wa joto.
Wan-Bissaka, ambaye pia yuko kwenye rada ya Galatasaray, ameachwa nyuma ya Diogo Dalot katika nafasi ya beki wa kulia.
United wako tayari kusikiliza ofa kwa wachezaji wao wengi ili kusaidia kufadhili usajili wa wachezaji wapya msimu huu wa joto mradi tu walingane na ubora na thamani yao.
Wanatafuta kusajili beki mpya wa kulia na kiungo wa kati ila McTominay na Wan-Bissaka ni miongoni mwa wachezaji ambao wanaweza kupatikana ikiwa bei yao itakuwa sawa.