Kwingineko

4 EPL kumgombea nyota Juve

KLABU za Tottenham, West Ham, Brighton na Everton zipanga kumsajili nyota wa Juventus Samuel Iling-Junior, mtandao wa Football Insider umesema.

Mkataba wa Iling-Junior, 20, utafikia kikomo majira ya kiangazi 2025 katika miamba hiyo ya Serie A, ambayo inasita kukubali kwamba huenda ikamuuza mshambuliaji huyo hodari kuepuka kumpoteza bura.

Timu hizo nne za Ligi Kuu England(EPL) zitatumia hitaji la Juventus kumuuza na kujaribu kupata saini ya nyota huyo wa timu ya taifa ya England chini ya miaka 21 majira yajayo ya kiangazi.

Kwa muda mrefu Spurs na Everton zimekuwa zikivutiwa na mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea na zilifikiria kumsajili wakati wa dirisha la uhamisho Januari, 2024.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button