Maguire aiganda United
Beki kisiki wa kikosi cha Manchester united Harry Maguire amesafisha hali ya hewa juu ya uwepo wa taarifa zilizomhusisha mchezaji huyo kipenzi cha mashabiki wa mashetani hao wekundu kuondoka viunga vya Old Trafford.
Maguire ameiambia Sky Sports kuwa viongozi wa klabu hiyo bado inahitaji huduma yake na anaiona ‘future’ yake katika timu hiyo washindi wa kombe la FA
“kusema ukweli ninachojua ni kuwa mimi ni sehemu ya kikosi hiki, nipo kwenye mipango yake kwa wakati ujao.” amesema
“Ninafuraha hapa, niko tayari muda wote kuipambania klabu hii, kuisaidia kushinda mataji makubwa” aliongeza
Mchezaji huyo mwenye miaka 31 ambaye kwa sasa anauguza majeraha ya misuli aliyoyapata Mei 6 mwaka huu alimaliza msimu wa ligi kuu ya England akiwa na magoli mawili na assist mbili akicheza mechi 22, 18 kati ya hizo akianza moja kwa moja.