Burudani

Madonna na Taylor Swift watawala MTV VMAs 2026

LOS ANGELES: WANAMUZIKI Madonna na Taylor Swift wamekuwa vinara wa Tuzo za MTV Video Music Awards (VMAs) 2026, baada ya kufanya vizuri katika hafla hiyo iliyofanyika Los Angeles, Marekani, huku wasanii hao wawili wakiondoka na tuzo muhimu.

Madonna, ambaye aliongoza kwa idadi ya tuzo, alitwaa tuzo saba, zikiwemo Mwanamuziki Bora wa Mwaka, Ushirikiano Bora na Sabrina Carpenter, pamoja na Mnenguaji Bora.

Ushindi huo uliendelea kuonesha nafasi yake katika historia ya VMAs.

Usiku huo pia ulikuwa wa kipekee kwa Madonna kwa kurejea kwenye jukwaa la VMAs kwa mara ya kwanza baada ya miaka 23. Alifungua hafla hiyo kwa onesho lililomshirikisha Sabrina Carpenter na baadaye Charli XCX.

Kwa upande wake, Taylor Swift alitwaa Video ya Mwaka kupitia wimbo wake wa ‘The Fate of Ophelia’, pamoja na tuzo ya Uongozi mzuri wa video ‘Opalite’ na ‘Tuzo ya Heshima ya Msanii muongozaji’, tuzo ya kwanza kutolewa katika kipengele hicho.

Ushindi huo ulimfanya Swift kufikisha tuzo 33 za VMAs katika kazi yake, na hivyo kuwa msanii aliyeongoza kwa idadi ya tuzo katika historia ya VMAs. Swift pia alitumia jukwaa hilo kuonesha kwa mara ya kwanza video ya wimbo wake mpya, Patient Zero.

Hafla hiyo iliyokuwa ikiongozwa na Snoop Dogg iliwakutanisha mastaa mbalimbali wa muziki, huku Madonna na Swift wakiwa miongoni mwa majina yaliyotawala mjadala wa burudani duniani kufuatia ushindi wao na matukio mbalimbali ya usiku huo.

Related Articles

Back to top button