Ligi Kuu

Kocha Azam alia na Bakari Shime

DAR ES SALAAM: KOCHA Mkuu wa Azam FC, Rachid Taoussi amesema kutokuwepo kikosini nyota wake, Nassor Saadun kumeathiri mipango yake kuelekea mchezo wao dhidi ya Ken Gold FC.

Taoussi amezungumza hayo leo katika mkutano na waandishi wa habari za michezo kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara unaochezwa kesho Uwanja wa Azam Complex, uliopo Chamazi, jijini dhidi ya Ken Gold.

Saadun amejumuishwa katika kikosi cha timu ya Taifa, Taifa Stars chini ya Kocha Bakari Shime kilichoingia kambini kujiandaa na michezo ya kufuzu fainali za Mataifa Bingwa Afrika CHAN dhidi ya Sudan.

Kocha huyo amesema kutokuwepo kwa Saadun analazimika kufanya mabadiliko katika kikosi cha timu yake kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Ken Gold kwa ajili ya kutafuta pointi tatu.

“Atawakosa baadhi ya wachezaji wake ambao wapo kwenye majukumu ya timu ya Taifa, akiwemo Saadun  ambaye amekuwa na kiwango bora kutokuwepo kutaathiri mipango yangu ya mechi ya kesho na kulazimika kufanya mabadiliko machache ya kikosi,” amesema kocha huyo.

Related Articles

Back to top button