Burudani

Vanessa Mdee afanyiwa upasuaji wa jicho Marekani

MAREKANI: MAMA wa watoto wawili ambaye ameachana na muziki wa bongo fleva, Vanessa Mdee amefanyiwa upasuaji wa macho akiwa nchini Marekani anakoishi kwa sasa.

Vanessa aliweka video kwenye ukurasa wake wa TikTok akiwa na mumewe Rotimi huku akiwa ameziba jicho kwa kitambaa, akiwaambia mashabiki wake kwamba anaendelea vyema baad ya upasuaji huo.

Vanessa katika video hiyo aliandika “Upasuaji wako wa jicho ulipofaulu, Utukufu kwa Mungu, “Mimi ni kipofu katika jicho moja lakini hiyo haijanizuia kutekeleza ndoto zangu,”

Katika ukuras wake wa Instagram Vanessa amesema changamoto ya macho alikuwa nayo tangu mwaka wa 2021.

“Nilipata tatizo lililofanya jicho langu moja kuwa kipofu, kwa muda nimekuwa nikitumia jicho moja, jingine ni kipofu, So ni ulemavu lakini it is not something naweza sema ni ulemavu kwa sababu Mungu amenijalia na jicho ambalo linaona, so it’s fine..”

Related Articles

Back to top button