Burudani

Steve Mweusi aomba sapoti ya serikali

MCHEKESHAJI maarufu nchini Steve Moses ‘Steve Mweusi’ ameelezea changamoto anazokutana nazo kwenye sanaa hiyo ikiwemo upungufu wa vitendai kazi, hivyo amemuomba Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ kuliangalia suala hilo.

Akizungumza na mwandishi wa mtandao huu mapema leo, Steve amesema mara kadhaa amekuwa akirudisha kwa jamii, na kwamba endapo atasaidiwa upatikanaji wa baadhi ya vifaa itasaidia kukuza timu yake, kukuza kipato na hatimaye kuendelea kusaidia jamii.

“Natamani serikali iniongezee vifaaa vya kushutia kamera ninayo moja ningepata kama tatu  ili kufanya kazi kwa uharaka zaidi niweze kutoa ajira kwa vijana zaidi,” amesema Steve.

Amesema atahakikisha anaendelea na dhamira yake ya kusaidia jamii ikiwemo vijana ambao mara kadhaa amekuwa akiwaunga mkono kwenye masuala mbalimbali.

“Nimewapa vijana pikipiki zaidi ya nane tangu nianze sanaa kama kukumbuka nilikotoka nao vijana ambao nimesota nao hapo zamani kwa sasa wanamaisha yao na wengine wameoa wanaendesha familia zao,” ameongeza Steve.

Related Articles

Back to top button