Tetesi

Liverpool, Real Madrid bado zamwinda Mbappé

TETESI za usajili zinasema Liverpool na Real Madrid ndizo zinaonesha nia kumsajili Kylian Mbappé kutoka Paris Saint-Germain huku mkataba wake na klabu hiyo ya Ufaransa ukimalizika mwisho wa msimu huu. Mfaransa huyo sasa yupo huru kuzungumza na klabu nyingine kuhusu makubaliano ya awali ya mkataba. (Le Parisien)

Fowadi mwingine ambaye yupo kwenye radi za Liverpool ni mfungaji hodari wa Wolves aliyeko kwenye kiwango kwa sasa Hwang Hee-chan, ambaye pia anawindwa na Tottenham Hotspur.(Football Insider)

Barcelona inaamini inaweza kumsajili kiungo Aleix Garcia kutoka Girona kwa nusu bei ya sasa ya pauni mil 21.9(Mundo Deportivo)

Manchester City ni miongoni mwa vilabu kadhaa zinavyomfuatilia beki Leny Yoro, 18, lakini timu yake ya Lille inataka ada ya pauni mil 78.(Le 10 Sport via Manchester Evening News)

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button