Tetesi

Lavia azigonganisha Liverpool, Arsenal na Chelsea

LIVERPOOL, Arsenal na Chelsea zote zimefanya mazungumzo kuhusu uwezekano wa usajili wa kiungo wa Southampton, Romeo Lavia.

Kwa Mujibu wa tovuti ya michezo, 90min Southampton inaamini kabisa kiungo huyo wa kimataifa wa Ubelgiji ana thamani ya pauni zaidi ya milioni 50 sawa na zaidi ya shilingi bilioni 149.

Klabu zote hizo zimeweka jina la Lavia mwenye umri wa miaka 19 katika orodha ya wachezaji zinazowahitaji.

Tayari Liverpool imeanza maboresho kwenye safu yake ya kiungo kwa kuwasajili Alexis Mac Allister and Dominik Szoboszlai lakini bado inahitaji usajili zaidi.

Arsenal inatarajiwa kutangaza usajili wa Declan Rice lakini wakati Granit Xhaka akiondoka na hatma ya Thomas Partey na Jorginho haijulikani, washika mtutu hao wana mpango wa kuboresha zaidi sehemu ya kiungo.

Chelsea inamwania kwa udi na uvumba Moises Caicedo na inaandaa ofa ya kwanza lakini bado inatafuta wachezaji wengine kutokana na eneo lake la kiungo kuhitaji maboresho kufuatia kuondoka kwa Mason Mount, Mateo Kovacic, Reben Loftus-Cheek na NG’olo Kante.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button