Burudani

Lamar ashinda tuzo 8 za BET Hip Hop 2024

LAS VEGAS: RAPA Kendrick Lamar ameshinda tuzo nane kwenye Tuzo za BET Hip Hop 2024, ukiwemo Wimbo Bora wa Mwaka.

Tuzo hizo zimetolewa alfajiri ya Oktoba 16, 2024 katika klabu ya Drai’s Beachclub & Nightclub huko Las Vegas, Nevada nchini Marekani.

Rapa huyo wa ‘Not Like Us’, ambaye ameshinda tuzo hizo kati ya tuzo 11 alizokuwa akishindania kupitia wimbo wake wa ‘Not Like Us.’

Baadhi ya vipengele alivyonyakua rapa huyo ni pamoja na ‘Msanii Bora wa Mwaka wa Hip-Hop’, ‘Wimbo Bora wa Mwaka’, ‘Video ya Muziki Bora ya Mwak’a’ na ‘Mwanamuziki Bora wa Mwaka’.

Lamar alikumbana na ushindani mkali katika kipengele cha Msanii Bora wa Mwaka, dhidi ya wasanii kama Drake, 21 Savage, Cardi B, Future, GloRilla, Megan Thee Stallion na Nicki Minaj.

Pia wimbo wa ‘Not Like That’ umeshinda wimbo wenye mafanikio wa mwaka. Wimbo huu ulifanya vizuri katika vitabu vya kuhifadhi rekodi kwa muda wa wiki 22 ukiwa namba moja kwenye chati ya nyimbo za rap Billboard.

Fat Joe, ambaye aliyekuwa mtangazaji, katika tuzo hizo alianza hafla hiyo kwa kucheza wimbo wake wa 2006 ‘Make It Rain’ akiwa pamoja na DJ Spinatik.

Baadhi ya wasanii waliotumbuiza katika hafla hiyo ni Trina, Yung Miami, Juicy J, 310babii, BossMan Dlow na 2 Chainz.

Baadhi ya wasanii wengine waliopata tuzo ni pamoja na Travis Scott aliyepata tuzo ya Msanii Bora wa Hip Hop wa Mwaka kupitia wimbo wake wa ‘I Am Hip Hop’ na 50Cent aliyepata tuzo ya ‘Hustler wa Mwaka’.

Related Articles

Back to top button