Mejja: Siri ya mafanikio yangu ni hii
NAIROBI: MSANII wa Gengetone kutoka Kenya Mejja ameweka wazi kwamba amedumu katika tasnia ya muziki na anaendelea kupata mikataba ya makampuni mbalimbali kwa sababu yeye ni wa kipekee.
Anasema amechagua kuwa wa kipekee, chaguo ambalo anaamini ni muhimu kwa thamani ya muda mrefu na hiyo ndiyo nguzo yake kuu kuelekea mafanikio yake.
“Somo moja muhimu ambalo nimejifunza kama msanii ni kwamba sanaa inapaswa kujitengeneza vyema. Kitu chochote adimu kina thamani zaidi. Ikiwa unakuwa wa kawaida sana, thamani yako inapungua,
“Ikifikiri kama watu wengine, thamani yako itapungua. Na Kadiri unavyokuwa wa kipekee, ndivyo mahitaji yanavyoongezeka. Lakini sio tu kuwa wakawaida, unahitaji muziki mzuri, tabia thabiti, na imani kwa sababu Mungu yu juu ya yote,” amesisitiza.
Akiwa kwenye tasnia ya muziki kwa miaka 17, Mejja pia aliwahutubia wakosoaji wa mashairi yake, akibainisha kuwa maoni ya wengine yanategemea umri na mtazamo wao.
“Baadhi ya watu hutengeneza nyimbo zinazofaa familia. Ninajaribu kuweka usawa, kwa kuwa nahitaji kuhudumia kila mtu. Lazima niandike juu ya vitu kama karamu, wanawake na pombe, kwa sababu ndivyo watu wanaelewa na kuhusiana navyo,” ameeleza Mejja.