Michezo Mingine

Kriketi kuanza kutimua vumbi leo

Msumbiji yamuhofia mwenyeji Tanzania

Mashindano ya Cricket World  Cup Africa Division 2 Qualifier kuanza kufanyika leo katika viwanja vya Gymkhana Posta jijini Dar es Salaam yakishirikisha nchi nane.

Akizungumza na Mratibu wa mashindano hayo, Mratibu wa  mashindano ya Kriketi Tanzania (TCA) Atif Salim amesema katika michuano hiyo Kuna timu nane na timu zimepangwa katika makundi mawili huku kila kundi likiwa na timu nne.

“Tanzania ipo kundi A ambapo itakuwa na Nigeria, Msumbiji na Malawi, huku kundi B likiundwa na Ghana, Botswana, Sierra Leone na Rwanda”, amesema Atif.

“Washindi wawili wa kila kundi watacheza nusu fainali, kisha fainali  na kutafuta mshindi wa tatu. Watakaocheza fainali tayari wote watakuwa wamefuzu kwenda Division I, na nchi itakayokuwa mshindi wa tatu nayo itafuzu kwenda mbele Division I,” amesema Atif.

Kwa upande wake Kocha wa timu ya kriketi ya Msumbiji, Filipe Cossa amesema  Tanzania ndio timu  inayoweza kumzuia katika mashindano ya kriketi ya kufuzu kombe la dunia, daraja la pili (Divisheni II) kwa vijana wenye umri chini ya miaka 19.

Michuano hiyo ambayo itashirikisha  jumla ya Mataifa nane, inatarajiwa kuanza leo kwenye viwanja vya Gymkhana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Kocha huyo amesema  anaihofia Tanzania kutokana na ubora wake na pia inacheza katika ardhi ya nyumbani.

“Kwa hali ilivyo Tanzania ndiyo timu  inaweza kutuzuia kufuzu kwa sababu inacheza nyumbani. Malengo yetu ni kufuzu kwenda Division I, tumejipanga kucheza kwa nidhamu na kutoa ushindani kwa wapinzani wetu,” amesema Cossa.

Naye Kocha Msaidizi wa timu ya kriketi ya vijana Tanzania, Salum Jumbe  amesema  wapo tayari kufuzu safari hii kutokana na maandalizi waliyofanya.

“Tunavijua viwanja vyote ambavyo tutatumia kwenye mashindano, vijana wako vizuri na safari hii hatutawaangusha Watanzania, tupo tayari kufuzu,” amesema Jumbe.

Kwa mujibu wa ratiba,mechi ya ufunguzi ni kati ya mwenyeji Tanzania itakayokutana na Nigeria kwenye viwanja vya Gymkhana.

Related Articles

Back to top button