Nyumbani
Uhamiaji vs Mashujaa kirafiki leo

TIMU ya Mashujaa ya Kigoma leo itacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Uhamiaji ya Zanzibar.
“Tutacheza mchezo mwingine wa kirafiki hii leo majira ya saa 10 jioni dhidi ya timu ya Uhamiaji Zanzibar,”imesema taarifa ya Mashujaa.
Tayari Mashujaa imecheza mmoja Zanzibar dhidi ya Mafunzo na kupoteza kwa magoli 3-2.
Mashujaa ipo Zanzibar kwa ajili ya maandalizi ya Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kupanda daraja.