Ligi KuuNyumbani

Ni patashika Mzizima Dabi leo

BAADA ya kipigo cha magoli 3-0 kutoka kwa Raja Casablanca katika mchezo Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba leo ni mwenyeji wa Azam ukiwa mchezo wa marudiano Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mchezo huo utapigwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Katika mchezo wa kwanza kati ya timu hizo uliofanyika Oktoba 27, 2022 Azam iliibuka mshindi dhidi ya Simba kwa goli 1-0 likifungwa na Prince Dube dakika 35.

Simba inashika nafasi ya 2 katika msimamo wa ligi kuu ikiwa na pointi 53 baada ya michezo 22 wakati Azam ni ya nne ikikusanya pointi 43.

Related Articles

Back to top button