NyumbaniTetesiWasifu

Job atuma salamu nzito Yanga

Mashabiki tulieni

DAR ES SALAAM: NAHODHA msaidizi wa Yanga, Dikson Job amewatumia ujumbe mashabiki wa timu hiyo kufuatia maumivu wanayopitia kutokana na vipigo mfululizo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Job amewaahidi furaha kwenye michezo ijayo akisema huu ni upepo mbaya unavuma kwao ila watasimama tena.

“Wananchi,
Poleni sana kwa kipindi kigumu tunachopitia, nafahamu maumivu haya yanachagizwa na ukweli kwamba mnaipenda kwa dhati timu yenu na mnatuamini sana wachezaji wenu.

Lakini msisahau wananchi, hakuna wakati sisi tunakua Imara kama pale tunapopitia magumu. Nyie mnakumbuka nyakati nyingi tulizozomewa na watu wote Tulisimama tena kwa matumaini na kuishangaza Dunia ya wapenda soka” ameandika Job na kuongeza

“Wananchi, Tuchane kalenda yenye kumbukumbu zote Mbaya na tuanze upya kwa Kasi na Tamaa ya kuendelea kuwafanya mjivunie kuwa mashabiki wa klabu bora zaidi kwenye taifa letu.”

Jumamosi Novemba 30, Yanga watashuka tena dimbani dhidi ya Namungo kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kabla ya kusafiri Kwenda Algeria kukipiga na MC Algers kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button