Mapinduzi CupNyumbani

Kivumbi Mapinduzi cup kuendelea leo

PATASHIKA ya mashindano ya Kombe la Mapinduzi inaendela leo kwa michezo miwili.

Yanga iliyopo kundi C itakamilisha mechi za makundi itakapomenyana na KVZ kwenye uwanja wa New Amaan Complex.

Nazo Mlandege na Chipukizi za kundi A zitakiwasha katika mchezo utakaotangulia kwenye uwanja huo huo.

Katika michezo miwili ya michuano hiyo iliyofanyika Januari 3, Simba imeichapa Singida Fountain Gate mabao 2-0 wakati APR imeibuka mshindi dhidi ya JKU kwa mabao 3-1.

Related Articles

Back to top button