Mastaa
Irene Uwoya: Hakuna mama anayetamani mtoto wake awe na tabia mbaya

DAR ES SALAAM: MUIGIZAJI wa filamu nchini Tanzania, Irene Uwoya, amesema kuwa hakuna mama mwenye nia mbaya au anayetamani mtoto wake akue katika malezi mabaya.
Akizungumza kuhusu malezi ya watoto, Uwoya amesisitiza kuwa si sahihi kuwahukumu wazazi au kuwanyooshea vidole watoto wa watu wengine kutokana na mienendo yao.
“Sio vizuri kumnyoshea kidole mtoto wa mwenzio, kwa sababu hakuna mama duniani aliyeingia leba akitaka mtoto wake awe kwenye malezi mabaya,” amesema Irene Uwoya.
Ameongeza kuwa kila mzazi hutamani mtoto wake akue katika mazingira mazuri na kuwa na maisha yenye mafanikio, hivyo jamii inapaswa kutoa ushauri na msaada badala ya hukumu kwa wazazi na watoto wao.




