Ligi Kuu

Hii ndio Yanga sasa

DODOMA: MASHABIKI wa Yanga wamekataa unyonge mtaani kwasasa wanasema chama lao limerejea baada ya kupitia misukosuko ya kukosa matokeo sasa ni kama wamerejea relini baada ushindi katika michezo miwili mfufulizo kwa mara ya kwanza tangu mwishoni mwa mwezi Oktoba.

Tangu Novemba 02, 2024 Yanga wamepitia kipindi kigumu ambapo walipopoteza bao 1-0 dhidi ya Azam Fc na kisha kutandikwa mabao 3-1 na Tabora United na baadae kupoteza 2-0 dhidi ya Al Hilal kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kabla ya kushinda 2-0 kwa Namungo Fc na kupoteza 2-0 nchini Algeria dhidi ya MC Algers.

Safari yenye machungu iliendelea kwa Wananchi kwani waliamini wataifunga TP Mazembe lakini waliambulia sare japo walijivunia kuwa timu imeanza kuupata muelekeo na ndipo walipokuja kupata ushindi dhidi ya Mashujaa Fc kabla ya jana kuitandika Prisons na kufanikisha ushindi miwili mfululizo.

Mashabiki wa Yanga mkoani Dodoma wamejitokeza kwa wingi kuipokea timu yao ilipowasili mkoani humo kwaajili ya mchezo wa Jumatano dhidi ya Dodoma Jiji.

 

Related Articles

Back to top button