Ligi Kuu

Salvatory Edward atua Pamba jiji FC

MWANZA: UONGOZI wa Pamba jiji FC, umewatambulisha aliyekuwa kocha wa timu ya Taifa ya watu wenye Ulemavu (Tembo Warriors), Salvatory Edward akiwa msaidizi wa Goran Kopunovic kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

Afisa Habari wa Pamba jiji FC, Martin Sawema ameiambia SpotiLeo kuwa  wamefanya maboresho ya benchi la ufundi kwa kuhakikisha wanapata watu wenye uzoefu na ligi ya Tanzania ili wafanikiwe malengo yao.

Amesema wamekamilisha zoezi la kuundaa benchi imara la ufundi likiongozwa na Goran anayeifahamu vizuri ligi kuu bara baada ya kufundisha soka la Tanzania, Salvatory aliyewahi kucheza Yanga na kufundisha baadhi ya timu mbalimbali kabla ya kukabidhiwa timu ya Taifa ya watu wenye Ulemavu.

“Tumefanikiwa kuimarisha benchi letu la ufundi, Goran atasaidiana na Salvatory pamoja na kocha wa viungo Kakooza Rogers, usajili unaendelea kufanyika kwa kuboresha kikosi chetu kwa msimu ujao,” amesema Sawema.

Amesema usajili unaendelea kulingana na mapendekezo ya kocha Mkuu (Goran) ya kujenga kikosi imara, kinacholeta ushindani mkubwa kwenye Ligi Kuu Bara msimu ujao.

Sawema amesema wamejiandaa vizuri hawataki kuwa mfano kwa timu zingine kwa msimu mmoja kupanda na kushuka kutokana na kushindwa kufanya vizuri katika ligi hiyo

Pambana jiji FC imerejea Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2024\ 25 baada ya miaka 23 tangu iliposhuka ligi hiyo 2001.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button