Tetesi

Nuno Santo kuinoa Nottingham Forest

KLABU ya Nottingham Forest siku chache zijazo inatarajiwa kumteua kocha wa zamani wa Wolves na Tottenham, Nuno Espirito Santo, huku mreno huyo, 49, akichukua nafasi ya Steve Cooper.(A Bola – in Portuguese)

Barcelona ipo tayari kusikiliza ofa za kumsajili winga wa Kibrazil Raphinha, 27, huku Manchester United ikifikiria kupendekeza mabadilishano yanayomhusisha mchezaji huyo za zamani wa Leeds United na Jadon Sancho. (Sport – in Spanish)

Tottenham imefanya mazungumzo kuhusu uwezekano wa uhamisho wa beki wa kati wa Nice na Ufaransa, 23, Jean-Clair Todibo. (Football.London)

Fulham inapima iwapo itume ombi kumsajili fowadi wa Nigeria, Akor Adams, 23, anayecheza Montpellier ya Ufaransa.(Football Insider)

Chelsea inajiandaa kumuuza beki wa kushoto Ian Maatsen dirisha la uhamisho Januari 2024 huku Manchester City, West Ham, Borussia Dortmund, Napoli na Roma zikiwa na nia kumsajili mdachi huyo mwenye umri wa miaka 21.(90min

Related Articles

Back to top button