Gor Mahia waharibu sherehe za Fountain Gate Fc
BABATI: UONGOZI wa timu ya Fountain Gate FC umetangaza rasmi silaha zao zitakazowapa burudani msimu wa 2024/25.
Silaha hizo zimetangazwa leo kwenye tamasha la sherehe za “The Tanzanite Fountain Gate Day”, lililofanyika katika dimba la Tanzanite Kwaraa uliopo, Babati, Manyara.
Mbali na utambulisho wa silaha hizo pia wameweka wazi kuwa watatumia wilaya ya Babati kucheza mechi zao za nyumbani wakitumia uwanja huo wa Tanzanite Kwaraa.
Sherehe hizo zilitamatishwa na mchezo wa kirafiki kati Fountain Gate FC dhidi ya Gor Mahia ya Kenya, wenyeji wamepoteza kwa bao 1-0.
Kikosi kilichotambulishwa na Ofisa habari wa timu hiyo Issa Mbuzi kinaundwa na John Noble, Oremade Olawale, Fikirini Bakari, Fadhili Anacret Kisunga, Anack Mtambi na Aron Lulambo.
Shafik Batambuze, Amos Kadililo, Laurian Makame, Mussa Habibu, Yessaya Hebron, Asi Serge, Abdallah Kurandana, Henrick Vitalis, Zam Kouffou, Abal Kassim, Nicolas Gyan, na Elie Mokono wanaongeza idadi ya silaha hizo.
Wengine ni Ediger William, John Kelwish, Selemani Mwalimu, Dickson Ambundo, Salum Kihimbwa, Patrick Lembo, Hashim Omary Kilemile, Bakari Francois Landry, Sadick Said, Arafat Ally, Abdulrazack Salum Athuman, Amos Nada na Hassan Mey.
Kamanda wa Jeshi hilo ni Mohammed Muya anayeongoza jeshi la kikosi cha timu hiyo na kutarajiwa kufanya makubwa zaidi msimu wa 2024/25 ambao wataanza mechi ya kwanza ugenini dhidi ya Namungo FC, agosti 16, mwaka huu dimba la Majaliwa, Ruangwa, Lindi.